Posts

TANA RIVER : BARAZA LA WANAHABARI NCHINI (MCK) LAHIMIZA USHIRIKIANO BAINA YA WANAHABARI NA UMMA

Image
NA DENNIS MAITHYA . Mratibu wa baraza la kitaifa la wanahabari nchini (MCK) eneo la pwani Bi. Maureen Mudi ametoa wito kwa wanahabari kuzingatia kanuni za uanahabari msimu huu wa uchaguzi ili kuhakikisha usawa wa utoaji habari . Akizungumza katika kongamano lililokutanisha mck, wanahabari na washikadau wengine mjini Hola kaunti ya Tana River, Mudi ameelezea umuhimu wa ushirikiano baina ya asasi mbalimbali za jamii na wahabari , pamoja na umma kufahamu utendakazi wa wanahabari. "Kongamano hili linakutanisha wananchi wa mashinani na wanahabari kuwaeleza utendakazi wa wanahabari na majukumu ya vyombo vya habari ikiwemo utoaji wa habari kwa njia zinazostahili ."   Mratibu huyo ameongeza kuwa baraza la kitaifa la wanahabari limeandaa misururu ya mafunzo kwa wanahabari uchaguzi mkuu unapowadia ili kuhakikisha wanaripoti matukio yanayohusiana na uchaguzi kwa njia ya usawa. "kama mck tumekuwa tukifanya mafunzo kwa wanahabari tunapoelekea uchaguzini.Himizo langu ni kwamba watoe ...

TANA RIVER : WANASIASA WAONYWA DHIDI YA SEMI ZA CHUKI NA KAMPENI ZA USIKU

Image
    Kamishna wa Tana River Thomas Sankei akiidhinisha msafara wa amani                                                                                       NA DENNIS MAITHYA                                                                                                                          Naibu   kamishna kaunti ya Tana River Joseph Lenkarie ameonya wanasiasa kaunti hiyo  dhidi ya semi za chuki na uchochezi  katika kipindi kilichosalia kabl...

WAFUGAJI SAMAKI TANA RIVER KUFAIDI SOKO MBADALA LA SAMAKI

Image
NA DENNIS MAITHYA Wafugaji wa samaki kaunti ya Tana River sasa watapata fursa ya soko jipya la bidhaa zao baada ya kufanyiwa  mafunzo ya njia mbadala za uuzaji wa nyama ya samaki kwa wateja wa ndani na nje ya kaunti. Kwa mujibu wa Numias Kiti, mkufunzi wa maswala ya uvuvi  kutoka shirika la Farm Africa , wakulima 112 wamepewa mafunzo ya kiufundi kuhusu ufugaji wa samaki huku wengine 105 wakipewa mafunzo ya kibiashara. Numias kiti -mkufunzi wa ufugaji samaki shirika la Farm Africa. Mafunzo hayo amesema yamehusisha kuunganisha wafugaji wa samaki na soko ambapo sasa wataweza kuuza samaki kwa njia  kama vile samosa,keki, kebab na baga, njia ambazo amesema zinaongeza thamani ya samaki na pia kuondolea wafugaji hasara ya samaki kuharibika haraka . "kwasasa tumefunza wakulima 112 mafunzo ya kiufundi na wengine 105 kuhusu biashara. pia tumekuwa na maonyesho ya mauzo mbadala ya bidhaa za samaki kama vile kebab, samosa na vinginevyo ambavyo vitapanua soko na pia kuongeza thamani y...

NG'OMBE 1,036 TANA RIVER KUCHINJWA KATIKA MPANGO WA SERIKALI KUKABILI MAKALI YA KIANGAZI NCHINI

Image
NA DENNIS MAITHYA Serikali kupitia shirika la msalaba mwekundu inalenga kununua na kuchinja ng’ombe 1,036 waliodhoofika  kaunti ya Tana River katika mpango wake wa kupunguza hasara kwa wafugaji kutokana na ukame ambao makali yake yanazidi kung'ata. (picha ya hifadhi:mzoga wa mfugo aliyekufa kutokana na ukame Tana River 2021) kwa mujibu wa mratibu wa shirika la msalaba mwekundu Tana River Gerald Bombe eneo la Tana Kaskazini ambalo limeathirika zaidi limetengewa asilimia 40 ya ng'ombe ambayo ni sawia na ng'ombe 414, Galole asilimia 35 ambayo ni ng'ombe 363 huku Delta ikipewa asilimia 25 ambayo ni ng'ombe 259. "kutokana na utathmini wa CSG Tana North imeathirika zaidi. Galole kwa wakati huu imeathirika zaidi kuliko delta tofauti na kawaida ambapo Delta huathirika lakini angalau imeshuhudia mvua kiasi kulinganishwa na maeneo mengine  "     picha hifadhi Mratibu wa shirika la msalaba mwekundu Gerald Bombe katika wadi ya wayu Bombe ameongeza kuwa idadi hiyo ya ...

BURA: WATOTO WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA KWENYE MKONDO WA MAJI

Image
NA DENNIS MAITHYA Watoto wawili wa kike walio na umri wa miaka 13 na 14 mtawalia wameripotiwa kufariki dunia eneo la Bura gatuzi dogo la Tana North kaunti ya Tana River baada ya kuzama kwenye mkondo wa kupitishia maji maeneo ya Nanighi. Kulingana na ripoti ya idara ya polisi Bura tarehe 24 Juni, wawili hao wakazi wa kata ndogo ya BilBil walikuwa wanaogelea kwenye mkondo huo wa maji walipokutana na mauti. Ripoti hiyo imesema kuwa msichana wa kwanza wa miaka 13 alizama akiokoa mtandio uliokuwa unabebwa na wimbi la maji huku mwenzake wa miaka 14 akizama alipokuwa akijaribu kumuokoa . Miili yao ilichukuliwa kufuata taratibu za kisheria. Idara hiyo sasa imetoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanaandamana na mtu mzima wanapoenda kuchota maji au kuogelea katika mikondo hiyo ya maji iliyoko Bura  kwani kiwango cha maji hupanda na kushuka na kuweka hatari kwa watoto.

POLISI TANA RIVER WAOMBEWA UCHAGUZI MKUU UKIWADIA

Image
NA DENNIS MAITHYA Maafisa wa Polisi kaunti ya Tana River wamefanyiwa maombi maalum wanapojiandaa kuhudumia taifa katika uchaguzi mkuu wa Agosti tisa mwaka huu. Kamanda wa polisi gatuzi dogo la Tana Kaskazini Ali Ndiema amesema ibada hiyo ya maombi imewafaa sana maafisa wa polisi wanapojiandaa kwa uchaguzi mkuu nchini. Ndiema amesema kuwa nyakati za ibada angalau maafisa hunawiri ki imani na hata kisaikolojia kwani wanapotangamana na wenzao wanabadilishana hisia na mawazo. " Ibada hizi huwaleta maafisa wa polisi pamoja kupata baraka,kujengeka kiroho na hata kisaikolojia, hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzini tumejazwa nguvu na bila shaka tunarajia uchaguzi mwema."   Ali Ndiema(katikati) kamanda wa polisi gatuzi dogo la Tana North.  Aidha amebaini kuwa maafisa wamepewa mwongozo tosha wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao katika uchaguzi kama tume ya uchaguzi IEBC inavyoelekeza. "Tumezungumza na maafisa wetu na wanafahamu wanavyotakikana kufanya kazi kuhakikisha uchaguzi s...

KAZI MTAANI YAREJEA.ZAIDI YA VIJANA 5,000 TANA RIVER KUFAIDI

Image
 Zaidi ya vijana elfu tano katika wadi 15 kaunti ya Tana River watanufaika na awamu ya tatu ya mpango wa Kazi mtaani. Akizindua mpango huo eneo la Mikinduni gatuzi dogo la Galole siku ya jumatatu tarehe 6 Juni , Kamishena wa kaunti Thomas Sankei amesema kuwa awamu hiyo itazingatia kuwafaidi watu wenye mahitaji maalum kuwakinga na changamoto za kiuchumi. kamishna wa Tana River Thomas Sankei akizindua kazi mtaani awamu ya tatu Sankei ameongeza kuwa mpango huo umejiri wakati mwafaka ambapo uchaguzi mkuu unawadia , akidokeza kuwa tofauti na awali vijana  pia watahusishwa katika mazungumzo ya kuleta amani na kutatua mizozo katika jamii. "Tunataka vijana wetu wawe mabalozi wema katika maswala ya maadili,kujenga amani na kutatua mizozo katika jamii.wakati huu wa uchaguzi tunataka tuelekeze watu hatutaki vurugu." wakiongozwa na Robert Buya vijana waliohudhuria wamepongeza serikali kwa kuregesha mpango huo kwani wangali wanatatizwa na changamoto za kiuchumi. Aidha amesihi serikali ku...