BURA: WATOTO WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA KWENYE MKONDO WA MAJI
NA DENNIS MAITHYA
Watoto wawili wa kike walio na umri wa miaka 13 na 14 mtawalia wameripotiwa kufariki dunia eneo la Bura gatuzi dogo la Tana North kaunti ya Tana River baada ya kuzama kwenye mkondo wa kupitishia maji maeneo ya Nanighi.
Kulingana na ripoti ya idara ya polisi Bura tarehe 24 Juni, wawili hao wakazi wa kata ndogo ya BilBil walikuwa wanaogelea kwenye mkondo huo wa maji walipokutana na mauti.
Ripoti hiyo imesema kuwa msichana wa kwanza wa miaka 13 alizama akiokoa mtandio uliokuwa unabebwa na wimbi la maji huku mwenzake wa miaka 14 akizama alipokuwa akijaribu kumuokoa .
Miili yao ilichukuliwa kufuata taratibu za kisheria.
Idara hiyo sasa imetoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanaandamana na mtu mzima wanapoenda kuchota maji au kuogelea katika mikondo hiyo ya maji iliyoko Bura kwani kiwango cha maji hupanda na kushuka na kuweka hatari kwa watoto.
Comments
Post a Comment