KAZI MTAANI YAREJEA.ZAIDI YA VIJANA 5,000 TANA RIVER KUFAIDI

 Zaidi ya vijana elfu tano katika wadi 15 kaunti ya Tana River watanufaika na awamu ya tatu ya mpango wa Kazi mtaani.

Akizindua mpango huo eneo la Mikinduni gatuzi dogo la Galole siku ya jumatatu tarehe 6 Juni , Kamishena wa kaunti Thomas Sankei amesema kuwa awamu hiyo itazingatia kuwafaidi watu wenye mahitaji maalum kuwakinga na changamoto za kiuchumi.

kamishna wa Tana River Thomas Sankei akizindua kazi mtaani awamu ya tatu

Sankei ameongeza kuwa mpango huo umejiri wakati mwafaka ambapo uchaguzi mkuu unawadia , akidokeza kuwa tofauti na awali vijana  pia watahusishwa katika mazungumzo ya kuleta amani na kutatua mizozo katika jamii.

"Tunataka vijana wetu wawe mabalozi wema katika maswala ya maadili,kujenga amani na kutatua mizozo katika jamii.wakati huu wa uchaguzi tunataka tuelekeze watu hatutaki vurugu."

wakiongozwa na Robert Buya vijana waliohudhuria wamepongeza serikali kwa kuregesha mpango huo kwani wangali wanatatizwa na changamoto za kiuchumi.

Aidha amesihi serikali kufanya mpango huo uwe wa kudumu kutokana na idadi kubwa ya vijana kaunti hii kukosa ajira.

"Tunaomba serikali hii kazi isiwe ya msimu tu. Vijana wengi wamesoma lakini bado wanahangaika kiuchumi kutokana na ukosefu wa ajira."

Kina mama waliohusishwa katika uzinduzi wa kazi mtaani

 Kadhalika wamesema kuwa mradi huo utawaondolea vijana hatari ya kuzama kwenye matumizi ya mihadarati na dawa za kulevya . 

Kina mama aidha kupitia Mwanabaraka Abdallah wamependekeza kuongezwa kwa mapato ya kazi hiyo kutokana na majukumu mengi waliyotwikwa wazazi ikiwemo ada za shuleni na gharama ya juu ya maisha.

"Tunaomba ikiwezekana tuongezewe pesa ,tuko na watoto wanaenda shule na gharama ya maisha imepanda sana."

Vijana wasafisha eneo la barabara kazi mtaani awamu ya tatu

 Katika awamu ya kwanza ya mradi huo zaidi ya vijana 2,800 kati ya umri wa miaka 18-35 katika manispaa ya Hola walifaidi mpango huo.

Comments

Popular posts from this blog

NG'OMBE 1,036 TANA RIVER KUCHINJWA KATIKA MPANGO WA SERIKALI KUKABILI MAKALI YA KIANGAZI NCHINI

TANA RIVER : BARAZA LA WANAHABARI NCHINI (MCK) LAHIMIZA USHIRIKIANO BAINA YA WANAHABARI NA UMMA

TANA RIVER : WANASIASA WAONYWA DHIDI YA SEMI ZA CHUKI NA KAMPENI ZA USIKU