NG'OMBE 1,036 TANA RIVER KUCHINJWA KATIKA MPANGO WA SERIKALI KUKABILI MAKALI YA KIANGAZI NCHINI

NA DENNIS MAITHYA


Serikali kupitia shirika la msalaba mwekundu inalenga kununua na kuchinja ng’ombe 1,036 waliodhoofika  kaunti ya Tana River katika mpango wake wa kupunguza hasara kwa wafugaji kutokana na ukame ambao makali yake yanazidi kung'ata.

(picha ya hifadhi:mzoga wa mfugo aliyekufa kutokana na ukame Tana River 2021)

kwa mujibu wa mratibu wa shirika la msalaba mwekundu Tana River Gerald Bombe eneo la Tana Kaskazini ambalo limeathirika zaidi limetengewa asilimia 40 ya ng'ombe ambayo ni sawia na ng'ombe 414, Galole asilimia 35 ambayo ni ng'ombe 363 huku Delta ikipewa asilimia 25 ambayo ni ng'ombe 259.

"kutokana na utathmini wa CSG Tana North imeathirika zaidi. Galole kwa wakati huu imeathirika zaidi kuliko delta tofauti na kawaida ambapo Delta huathirika lakini angalau imeshuhudia mvua kiasi kulinganishwa na maeneo mengine " 
   picha hifadhi Mratibu wa shirika la msalaba mwekundu Gerald Bombe katika wadi ya wayu


Bombe ameongeza kuwa idadi hiyo ya kimaeneo imegawanywa zaidi katika wadi mbalimbali katika magatuzi hayo madogo kulingana na athari za ukame kiangazi katika  maeneo hayo kwa mfano, eneo la Galole limetengea wadi ya wayu iliyoathirika zaidi ng'ombe 163 , Kinakomba 109,chewani 55 na mikinduni 36. 

Mratibu huyo amesema kuwa mpango huo unalenga wafugaji kwa ujumla wanaohofia kuwa huenda mifugo wao washindwe kustahimili kiangazi.

 "Mpango huu unalenga yeyote ambaye ni mfugaji na anahofia huenda mifugo wake washindwe kustahimili makali ya kiangazi kufikia mwezi wa oktoba.Anaweza akatoa ng'ombe mmoja au mbuzi ama kondoo 5"
(picha hifadhi:wafugaj wamwinua ng'ombe aliyedhoofika kutokana na makali ya ukame)


Ng'ombe mmoja atanunuliwa kwa shilingi elfu kumi na tano( 15,000) huku  mbuzi au kondoo akinunuliwa kwa shilingi elfu tatu(3,000). Ng'ombe mmoja alengwa kulisha familia kumi , kondoo au mbuzi kulisha familia nne.

Tana River ni mojawapo ya kaunti 14 nchini ambazo mpango huo utatekelezwa.

Aidha Shirika la msalaba mwekundu litaendeleza mpango mwingine wa msaada wa kifedha kwa familia mia nane (800) kaunti hii huku kila familia ikilengwa kupewa shilingi elfu tano mia nne ishirini na nne (5,424.) Eneo la Delta familia 350 zitafaidi,Galole 250 na Tana kaskazini 250.

Bombe ameongeza kuwa angalau watu elfu sitini na tatu (63,000) kaunti hii kutokana na tathmini  ya mwisho wangali na hitaji la msaada wa dharura wa chakula, maji na mahitaji mengine msingi kukabili kiangazi.

Comments

  1. Wazo zuri japo idadi hiyo ya ng'ombe watakaochinjwa ingali chino mno,wangeongeza wafike angalau ng'ombe elfu mbili na pia wanunue kila ng'ombe kwa shilingi elfu kumi na saba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndiposa mfugaji amepewa hiari kati ya ng'ombe au mbuzi ama kondoo iwapo bei ya ng'ombe sokoni huenda ikawa juu ya kiwango serikali inachonunua.

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TANA RIVER : BARAZA LA WANAHABARI NCHINI (MCK) LAHIMIZA USHIRIKIANO BAINA YA WANAHABARI NA UMMA

TANA RIVER : WANASIASA WAONYWA DHIDI YA SEMI ZA CHUKI NA KAMPENI ZA USIKU