Posts

BURA: WATOTO WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA KWENYE MKONDO WA MAJI

Image
NA DENNIS MAITHYA Watoto wawili wa kike walio na umri wa miaka 13 na 14 mtawalia wameripotiwa kufariki dunia eneo la Bura gatuzi dogo la Tana North kaunti ya Tana River baada ya kuzama kwenye mkondo wa kupitishia maji maeneo ya Nanighi. Kulingana na ripoti ya idara ya polisi Bura tarehe 24 Juni, wawili hao wakazi wa kata ndogo ya BilBil walikuwa wanaogelea kwenye mkondo huo wa maji walipokutana na mauti. Ripoti hiyo imesema kuwa msichana wa kwanza wa miaka 13 alizama akiokoa mtandio uliokuwa unabebwa na wimbi la maji huku mwenzake wa miaka 14 akizama alipokuwa akijaribu kumuokoa . Miili yao ilichukuliwa kufuata taratibu za kisheria. Idara hiyo sasa imetoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanaandamana na mtu mzima wanapoenda kuchota maji au kuogelea katika mikondo hiyo ya maji iliyoko Bura  kwani kiwango cha maji hupanda na kushuka na kuweka hatari kwa watoto.

POLISI TANA RIVER WAOMBEWA UCHAGUZI MKUU UKIWADIA

Image
NA DENNIS MAITHYA Maafisa wa Polisi kaunti ya Tana River wamefanyiwa maombi maalum wanapojiandaa kuhudumia taifa katika uchaguzi mkuu wa Agosti tisa mwaka huu. Kamanda wa polisi gatuzi dogo la Tana Kaskazini Ali Ndiema amesema ibada hiyo ya maombi imewafaa sana maafisa wa polisi wanapojiandaa kwa uchaguzi mkuu nchini. Ndiema amesema kuwa nyakati za ibada angalau maafisa hunawiri ki imani na hata kisaikolojia kwani wanapotangamana na wenzao wanabadilishana hisia na mawazo. " Ibada hizi huwaleta maafisa wa polisi pamoja kupata baraka,kujengeka kiroho na hata kisaikolojia, hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzini tumejazwa nguvu na bila shaka tunarajia uchaguzi mwema."   Ali Ndiema(katikati) kamanda wa polisi gatuzi dogo la Tana North.  Aidha amebaini kuwa maafisa wamepewa mwongozo tosha wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao katika uchaguzi kama tume ya uchaguzi IEBC inavyoelekeza. "Tumezungumza na maafisa wetu na wanafahamu wanavyotakikana kufanya kazi kuhakikisha uchaguzi s...

KAZI MTAANI YAREJEA.ZAIDI YA VIJANA 5,000 TANA RIVER KUFAIDI

Image
 Zaidi ya vijana elfu tano katika wadi 15 kaunti ya Tana River watanufaika na awamu ya tatu ya mpango wa Kazi mtaani. Akizindua mpango huo eneo la Mikinduni gatuzi dogo la Galole siku ya jumatatu tarehe 6 Juni , Kamishena wa kaunti Thomas Sankei amesema kuwa awamu hiyo itazingatia kuwafaidi watu wenye mahitaji maalum kuwakinga na changamoto za kiuchumi. kamishna wa Tana River Thomas Sankei akizindua kazi mtaani awamu ya tatu Sankei ameongeza kuwa mpango huo umejiri wakati mwafaka ambapo uchaguzi mkuu unawadia , akidokeza kuwa tofauti na awali vijana  pia watahusishwa katika mazungumzo ya kuleta amani na kutatua mizozo katika jamii. "Tunataka vijana wetu wawe mabalozi wema katika maswala ya maadili,kujenga amani na kutatua mizozo katika jamii.wakati huu wa uchaguzi tunataka tuelekeze watu hatutaki vurugu." wakiongozwa na Robert Buya vijana waliohudhuria wamepongeza serikali kwa kuregesha mpango huo kwani wangali wanatatizwa na changamoto za kiuchumi. Aidha amesihi serikali ku...

MGOMBEA WA KITI CHA UWAKILISHI WA WANAWAKE ABUBUJIKWA NA MACHOZI KATIKA KITUO CHA IEBC

Image
NA DENNIS MAITHYA Mgombea wa kiti cha uwakilishi wa wanawake Tana River Bi. Mwanahamisi Omar alitekwa na hisia na kutokwa na chozi la furaha akikabidhiwa cheti na mkuu wa uchaguzi kaunti hiyo Yonah Ogalo. Mwanahamisi anayegombea kiti hicho kwa mara ya kwanza kwa tiketi ya chama cha Safina amesema kuwa pindi tu akikabidhiwa cheti hicho alimkumbuka marehemu baba yake ambaye alitamani sana kuwa naye kushuhudia ushindi wa mwanawe. Mwanahamisi Omar akipokezwa cheti na mkuu wa uchaguzi Yonah Ogalo "Nilipokuwa nakabidhiwa cheti nilitamani na kuhisi ningekuwa na baba yangu kando yangu.Hisia kidogo ya kumkumbuka ilinishika kwani ni siku kama ya tano hivi tangu nimpoteze."  Mwanahamisi ameahidi kuweka elimu ya mtoto wa kike kipaumbele akizingatia changamoto kama vile mimba na ndoa utotoni zinazowakumba watoto wa kike kaunti ya Tana River. "Sitakubali msichana kukatiza ndoto yake ya elimu kwasababu ya mimba .nitahakikisha wamesoma kwasababu wengi wametelekezwa na kuwachishwa shul...

TANA RIVER :WAGOMBEA 10 WA USENETA WAIDHINISHWA RASMI , TATU WAKIFUNGIWA NJE

Image
 Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC  imeidhinisha wanasiasa kumi pekee kuwania kiti cha useneta kaunti ya Tana River katika uchaguzi mkuu ujao. Meneja wa uchaguzi Yonah Ogalo amesema kuwa kumi hao ndio watakaogombea kiti hicho baada ya stakabadhi zao kukaguliwa na kudhibitishwa uhalali wao kuwania. Yonah Ogalo, meneja wa uchaguzi Tana River Kumi hao ni seneta wa sasa Juma Wario atakayewania kupitia tiketi ya chama cha ODM, Danson Mungatana aliyekuwa mbunge wa Garsen atakayewania kupitia chama cha UDA. Hassan Dukicha aliyekuwa mbunge wa Galole ambaye atawania kupitia Jubilee,Ali Bule aliyekuwa seneta wa kwanza atakayewania kupitia FPK na Jire Siyat ambaye alikuwa naibu gavana wa Tana River ambaye sasa atawania kupitia FORD Kenya. Juma wario(pili kutoka kulia) akipokea cheti kutoka meneja wa uchaguzi Yonah Ogalo Wengingine ni Alice Nakapwepwe, mwanamke wa kipekee kwenye kinyang'anyiro hicho kupitia chama cha Justice and Freedom party of Kenya na Sadam Salat wa ANC. Ali...

TANA RIVER: WAGOMBEA TANO KATI YA 12 WANAOWANIA KITI CHA SENETI WAIDHINISHWA RASMI NA IEBC KUFIKIA SIKU YA PILI

Image
NA DENNIS MAITHYA  Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kwa siku ya pili imeendelea kukagua stakabadhi za wanasiasa wanaowania viti mbalimbali vya kisiasa ili kuwaidhinisha rasmi kama wagombea wa viti hivyo. Kufikia leo jioni tarehe 30 Mei,  meneja wa uchaguzi kaunti ya Tana River Yonah Ogalo amedhibitisha tume hiyo kuidhinisha rasmi wagombea tano wa kiti cha seneti, idadi hiyo ikiwa ni asilimia 41.6 ya jumla ya wawaniaji kumi na wawili wanaotarajiwa kuwasilisha stakabadhi zao. Yonah Ogalo , meneja wa uchaguzi Tana River akiongea na wanahabari kwenye kituo cha kuidhinisha maseneta. Miongoni mwa wagombea tano wa useneti walioidhinishwa rasmi kufikia sasa ni aliyekuwa seneta wa kwanza wa  Tana River Ali Bule anayewania kupitia chama cha Federal Party  of Kenya (FPK). Ali Bule aliyekuwa seneta wa Tana River Danson Mungata , aliyekuwa mbunge wa Garsen ambaye sasa anawania useneta kupitia chama cha UDA kilicho kwenye muungano wa Kenya kwanza chini ya uongozi wa na...

SIKU YA USAFI WA HEDHI DUNIANI: WADAU TANA RIVER WATAKA HAMASA KUFANYWA ZAIDI MASHINANI.

Image
watoto wa kike wafurahia kupokea sodo na sabuni katika maadhimisho ya siku ya usafi wa hedhi. NA DENNIS MAITHYA. Huku ulimwengu mzima ukiadhimisha siku ya usafi wa hedhi , Kaunti ya Tana River imeungana na maeneo mengine kuadhimisha siku hiyo katika shule ya msingi ya Kalkacha, kata ya Kalkacha gatuzi dogo la Tana River. Hafla hiyo imevutia wasichana kutoka eneo hilo na viunga vyake, wengi wakiwa na matarajio ya kuelimishwa kuhusu usafi wa hedhi na angalau kupata sodo kama ishara ya kuashiria usafi wa hedhi. Chifu wa eneo hilo Osman Dara amebaini kuwa changamoto za siku za hedhi huwafanya wasichana wengi eneo hilo kutohudhuria shule, sababu zikiwemo kukosa sodo au hedhi kuchukuliwa kwa usiri. "Watoto wakiwa katika hali hizo wengi hawaendi shule , jambo hilo pia huchukuliwa kwa usiri mkubwa halizungumziwi na wazazi." Amesema Osman.   Chifu kalkacha Osman Dara  Kulingana na afisa wa afya ya uzazi katika hospitali ya rufaa ya Hola daktari Hawa Abdulghafoor , siku hii ina umuhim...