MGOMBEA WA KITI CHA UWAKILISHI WA WANAWAKE ABUBUJIKWA NA MACHOZI KATIKA KITUO CHA IEBC


NA DENNIS MAITHYA

Mgombea wa kiti cha uwakilishi wa wanawake Tana River Bi. Mwanahamisi Omar alitekwa na hisia na kutokwa na chozi la furaha akikabidhiwa cheti na mkuu wa uchaguzi kaunti hiyo Yonah Ogalo.

Mwanahamisi anayegombea kiti hicho kwa mara ya kwanza kwa tiketi ya chama cha Safina amesema kuwa pindi tu akikabidhiwa cheti hicho alimkumbuka marehemu baba yake ambaye alitamani sana kuwa naye kushuhudia ushindi wa mwanawe.

Mwanahamisi Omar akipokezwa cheti na mkuu wa uchaguzi Yonah Ogalo


"Nilipokuwa nakabidhiwa cheti nilitamani na kuhisi ningekuwa na baba yangu kando yangu.Hisia kidogo ya kumkumbuka ilinishika kwani ni siku kama ya tano hivi tangu nimpoteze."

 Mwanahamisi ameahidi kuweka elimu ya mtoto wa kike kipaumbele akizingatia changamoto kama vile mimba na ndoa utotoni zinazowakumba watoto wa kike kaunti ya Tana River.

"Sitakubali msichana kukatiza ndoto yake ya elimu kwasababu ya mimba .nitahakikisha wamesoma kwasababu wengi wametelekezwa na kuwachishwa shule kwasababu ya mimba."

Mwanahamisi Omar (mbele) akionyesha cheti 


 Aidha amedokeza kuwa atawapa kipaumbele wakunga wa kienyeji ambao anasema tangu jadi wamekuwa wakisaidia kinamama kujifungua , wengine akisema wamekuwa ustadi na tajriba katika nyanja hiyo hivyo kuna haja ya kuwatambua kwa mchango wao katika jamii.

Zaidi ya hayo ameahidi kuimarisha kilimo kwa kushirikiana na viongozi wengine panapostahili ili kuimarisha kilimo cha kaunti hii kwani ni mojawapo ya njia za kubuni ajira kwa vijana na kinamama.

"Nikipata nafasi hiyo nirashirikiana na viongozi wengine kuimarisha kilimo.mchanga wetu haujapimwa lakini hata kwa macho umedhihirisha uwezo wa kuzalisha sio cash crop sio food crop"

 Katika siku ya kwanza ya ukaguzi wa wanaoazimia kiti hicho cha uwakilishi wa wanawake, IEBC iliwapa vyeti rasmi wagombea wanne.

Alitangulia Amina Dika wa KANU, Sadia Halima Koro wa UDM,Ralia Buyotu wa TND na Mwanahamisi Omar wa SAFINA.


Ralia Buyotu wa TND akipokezwa cheti na Yonah Ogalo, mkuu wa uchaguzi Tana River.

Zoezi la ukaguzi litaendelea leo kwa siku ya pili huku wawaniaji wanne wakitarajiwa kuwasilisha stakabadhi zao.



Comments

Popular posts from this blog

NG'OMBE 1,036 TANA RIVER KUCHINJWA KATIKA MPANGO WA SERIKALI KUKABILI MAKALI YA KIANGAZI NCHINI

TANA RIVER : BARAZA LA WANAHABARI NCHINI (MCK) LAHIMIZA USHIRIKIANO BAINA YA WANAHABARI NA UMMA

TANA RIVER : WANASIASA WAONYWA DHIDI YA SEMI ZA CHUKI NA KAMPENI ZA USIKU