TANA RIVER :WAGOMBEA 10 WA USENETA WAIDHINISHWA RASMI , TATU WAKIFUNGIWA NJE
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeidhinisha wanasiasa kumi pekee kuwania kiti cha useneta kaunti ya Tana River katika uchaguzi mkuu ujao.
Meneja wa uchaguzi Yonah Ogalo amesema kuwa kumi hao ndio watakaogombea kiti hicho baada ya stakabadhi zao kukaguliwa na kudhibitishwa uhalali wao kuwania.
Yonah Ogalo, meneja wa uchaguzi Tana River |
Kumi hao ni seneta wa sasa Juma Wario atakayewania kupitia tiketi ya chama cha ODM, Danson Mungatana aliyekuwa mbunge wa Garsen atakayewania kupitia chama cha UDA.
Hassan Dukicha aliyekuwa mbunge wa Galole ambaye atawania kupitia Jubilee,Ali Bule aliyekuwa seneta wa kwanza atakayewania kupitia FPK na Jire Siyat ambaye alikuwa naibu gavana wa Tana River ambaye sasa atawania kupitia FORD Kenya.
Juma wario(pili kutoka kulia) akipokea cheti kutoka meneja wa uchaguzi Yonah Ogalo |
Wengingine ni Alice Nakapwepwe, mwanamke wa kipekee kwenye kinyang'anyiro hicho kupitia chama cha Justice and Freedom party of Kenya na Sadam Salat wa ANC.
Alice Nakapwepwe mwanamke wa pekee kwenye kinyang'anyiro cha useneta |
Pia kuna Hantiro Barako wa chama cha NARC Kenya , Bakari Garise wa chama cha PAA na Abdulaziz Soba wa UDP.
Hantiro Barako (kushoto) wa NARC kenya |
Meneja wa uchaguzi Yonah Ogalo amebaini kuwa zoezi la kukagua maseneta limekamilika na endapo kuna mwengine atakayejiwasilisha baadae itabidi awe na agizo la Mahakama. Kulingana naye kuna wawaniaji watatu ambao hawakufika kukaguliwa.
"Akija mwengine kesho baada ya kukamilika kwa zoezi hili itabidi awe na agizo la mahakama" Alisema.
Kumi hao waliofuzu wako huru kufanya kampeni zao huku wakihimizwa kufanya kampeni hizo kwa amani.
Zoezi la kukagua wawakilishi wa wanawake bungeni linaanza leo tarehe 1/06/2022 hadi tarehe tatu mwezi uu huu kabla ya kupisha magavana kukaguliwa.
Senator Bwanamaka nae vipi
ReplyDeleteKwa mujibu wa IEBC kumi waliotajwa ndio waliofuzu. Kwa mengi zaidi follow upate taarifa kadri zinapochipuka.
DeleteCan you please help me with information of women reps and mps cleared in Tana River?
DeleteAbdala bwanamaka matapu jina lake sioni ama akona shida
ReplyDeleteHakukaguliwa wakati wa zoezi ukaguzi wa wawaniaji wa useneta
Delete