KAZI MTAANI YAREJEA.ZAIDI YA VIJANA 5,000 TANA RIVER KUFAIDI
Zaidi ya vijana elfu tano katika wadi 15 kaunti ya Tana River watanufaika na awamu ya tatu ya mpango wa Kazi mtaani. Akizindua mpango huo eneo la Mikinduni gatuzi dogo la Galole siku ya jumatatu tarehe 6 Juni , Kamishena wa kaunti Thomas Sankei amesema kuwa awamu hiyo itazingatia kuwafaidi watu wenye mahitaji maalum kuwakinga na changamoto za kiuchumi. kamishna wa Tana River Thomas Sankei akizindua kazi mtaani awamu ya tatu Sankei ameongeza kuwa mpango huo umejiri wakati mwafaka ambapo uchaguzi mkuu unawadia , akidokeza kuwa tofauti na awali vijana pia watahusishwa katika mazungumzo ya kuleta amani na kutatua mizozo katika jamii. "Tunataka vijana wetu wawe mabalozi wema katika maswala ya maadili,kujenga amani na kutatua mizozo katika jamii.wakati huu wa uchaguzi tunataka tuelekeze watu hatutaki vurugu." wakiongozwa na Robert Buya vijana waliohudhuria wamepongeza serikali kwa kuregesha mpango huo kwani wangali wanatatizwa na changamoto za kiuchumi. Aidha amesihi serikali ku...