IEBC KUKAGUA STAKABADHI ZA WANAOAZIMIA VITI VYA KISIASA TANARIVER
Kutoka kulia kamishna wa TanaRiver Thomas Sankei, Yonah Ogalo mkuu wa uchaguzi TanaRiver, Omar Dhadho mkuu wa kitengo cha askari wa kaunti. |
NA DENNIS MAITHYA
Jumla ya wanasiasa 14 kaunti ya Tana River wanaazimia kugombea kiti cha ugavana kaunti ya Tana River.
Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa uchaguzi kaunti hii Yonah Ogalo ambaye amebaini kuwa tarehe 29 mwezi huu wanasiasa hao wanatarajiwa kuwasilisha stakabadhi zao kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kukaguliwa kabla ya kuidhinishwa rasmi kama wagombea wa viti hivyo.
Katika nafasi kiti cha useneta, wanasiasa 12 wameonyesha azma yao , idadi sawa na wanaowania kiti cha uwakilishi wa wanawake.
Huku kipindi cha kampeni aidha kikitarajiwa kuanza rasmi tarehe io hiyo 29 mwezi huu wa Mei na kuendelea kwa siku sitini, mkuu huyo amewasihi wanasiasa kufanya kampeni za Amani na pia wanaowania viti mbalimbali kupewa fursa ya kuomba kura kwani wana haki kikatiba.
Aidha ametoa wito kwa jamii kukumbatia na kuwapa nafasi wanawake na vijana ambao wamejitosa katika ulingo huo wa kisiasa kuwania nafasi za uongozi ili kuleta usawa huku akisisitiza umuhimu wa wakenya kujitokeza kushiriki kupiga kura siku ya uchaguzi ikiwadia.
Mkuu huyo amesema hayo katika kikao cha majadiliano kuhusu utayarifu wa kaunti ya TanaRiver katika uchaguzi mkuu unaojiri.
Mbivu na mbichi itabainika
ReplyDelete