Posts

Showing posts from May, 2022

TANA RIVER :WAGOMBEA 10 WA USENETA WAIDHINISHWA RASMI , TATU WAKIFUNGIWA NJE

Image
 Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC  imeidhinisha wanasiasa kumi pekee kuwania kiti cha useneta kaunti ya Tana River katika uchaguzi mkuu ujao. Meneja wa uchaguzi Yonah Ogalo amesema kuwa kumi hao ndio watakaogombea kiti hicho baada ya stakabadhi zao kukaguliwa na kudhibitishwa uhalali wao kuwania. Yonah Ogalo, meneja wa uchaguzi Tana River Kumi hao ni seneta wa sasa Juma Wario atakayewania kupitia tiketi ya chama cha ODM, Danson Mungatana aliyekuwa mbunge wa Garsen atakayewania kupitia chama cha UDA. Hassan Dukicha aliyekuwa mbunge wa Galole ambaye atawania kupitia Jubilee,Ali Bule aliyekuwa seneta wa kwanza atakayewania kupitia FPK na Jire Siyat ambaye alikuwa naibu gavana wa Tana River ambaye sasa atawania kupitia FORD Kenya. Juma wario(pili kutoka kulia) akipokea cheti kutoka meneja wa uchaguzi Yonah Ogalo Wengingine ni Alice Nakapwepwe, mwanamke wa kipekee kwenye kinyang'anyiro hicho kupitia chama cha Justice and Freedom party of Kenya na Sadam Salat wa ANC. Alice Na

TANA RIVER: WAGOMBEA TANO KATI YA 12 WANAOWANIA KITI CHA SENETI WAIDHINISHWA RASMI NA IEBC KUFIKIA SIKU YA PILI

Image
NA DENNIS MAITHYA  Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kwa siku ya pili imeendelea kukagua stakabadhi za wanasiasa wanaowania viti mbalimbali vya kisiasa ili kuwaidhinisha rasmi kama wagombea wa viti hivyo. Kufikia leo jioni tarehe 30 Mei,  meneja wa uchaguzi kaunti ya Tana River Yonah Ogalo amedhibitisha tume hiyo kuidhinisha rasmi wagombea tano wa kiti cha seneti, idadi hiyo ikiwa ni asilimia 41.6 ya jumla ya wawaniaji kumi na wawili wanaotarajiwa kuwasilisha stakabadhi zao. Yonah Ogalo , meneja wa uchaguzi Tana River akiongea na wanahabari kwenye kituo cha kuidhinisha maseneta. Miongoni mwa wagombea tano wa useneti walioidhinishwa rasmi kufikia sasa ni aliyekuwa seneta wa kwanza wa  Tana River Ali Bule anayewania kupitia chama cha Federal Party  of Kenya (FPK). Ali Bule aliyekuwa seneta wa Tana River Danson Mungata , aliyekuwa mbunge wa Garsen ambaye sasa anawania useneta kupitia chama cha UDA kilicho kwenye muungano wa Kenya kwanza chini ya uongozi wa naibu Rais William Ru

SIKU YA USAFI WA HEDHI DUNIANI: WADAU TANA RIVER WATAKA HAMASA KUFANYWA ZAIDI MASHINANI.

Image
watoto wa kike wafurahia kupokea sodo na sabuni katika maadhimisho ya siku ya usafi wa hedhi. NA DENNIS MAITHYA. Huku ulimwengu mzima ukiadhimisha siku ya usafi wa hedhi , Kaunti ya Tana River imeungana na maeneo mengine kuadhimisha siku hiyo katika shule ya msingi ya Kalkacha, kata ya Kalkacha gatuzi dogo la Tana River. Hafla hiyo imevutia wasichana kutoka eneo hilo na viunga vyake, wengi wakiwa na matarajio ya kuelimishwa kuhusu usafi wa hedhi na angalau kupata sodo kama ishara ya kuashiria usafi wa hedhi. Chifu wa eneo hilo Osman Dara amebaini kuwa changamoto za siku za hedhi huwafanya wasichana wengi eneo hilo kutohudhuria shule, sababu zikiwemo kukosa sodo au hedhi kuchukuliwa kwa usiri. "Watoto wakiwa katika hali hizo wengi hawaendi shule , jambo hilo pia huchukuliwa kwa usiri mkubwa halizungumziwi na wazazi." Amesema Osman.   Chifu kalkacha Osman Dara  Kulingana na afisa wa afya ya uzazi katika hospitali ya rufaa ya Hola daktari Hawa Abdulghafoor , siku hii ina umuhim

TANARIVER KAUNTI YA 4 KENYA KUZINDUA MWONGOZO UTAKAOSAIDIA KUKOMESHA UKEKETAJI

Image
( Kutoka kushoto) Abas Kunyo waziri jinsia Tana River,Thomas Sankei kamishna wa Tana River,Nyerere Kutwa Anti fgm Board na Khalif Hassan mkurugenzi wa elimu Tana River NA DENNIS MAITHYA Kaunti ya Tana River imekuwa kaunti ya hivi karibuni baada ya kaunti za Kisii, Migori na Garissa kuzindua mwongozo wa kukabiliana na ukeketaji.  Haya yamejiri baada ya kaunti hii Alhamisi tarehe 26 Mei 2022 kuzindua mwongozo wa kukabiliana na ukeketaji hadi mwaka 2025. Kulingana na ripoti moja ya shirika la UNICEF inakisiwa kwamba karibu wasichana na wanawake milioni 200 katika mataifa zaidi ya 30 duniani wamekeketwa. Ripoti hiyo aidha inaonyesha hapa kenya karibu wasichana na wanawake milioni tisa na laki tatu wamekeketwa. Kwa mujibu wa ripoti nyingine ya mwaka 2014 ya afya ya watu nchini (KDHS 2014) kiwango cha ukeketaji hapa nchini kwa wasichana na wanawake kati ya miaka 15 hadi 49 ilikuwa asilimia 21 mwaka 2014. Hapa Tana River kiwango cha ukeketaji ni asilimia 58 kulingana na ripoti hiyo huku jami

IEBC KUKAGUA STAKABADHI ZA WANAOAZIMIA VITI VYA KISIASA TANARIVER

Image
Kutoka kulia kamishna wa TanaRiver Thomas Sankei, Yonah Ogalo mkuu wa uchaguzi TanaRiver, Omar Dhadho mkuu wa kitengo cha askari wa kaunti. NA DENNIS MAITHYA Jumla ya wanasiasa 14 kaunti ya Tana River wanaazimia kugombea kiti cha ugavana kaunti ya Tana River.  Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa uchaguzi kaunti hii Yonah Ogalo ambaye amebaini kuwa tarehe 29 mwezi huu wanasiasa  hao wanatarajiwa kuwasilisha stakabadhi zao kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kukaguliwa kabla ya  kuidhinishwa rasmi kama wagombea wa viti hivyo. Katika nafasi kiti cha useneta, wanasiasa 12 wameonyesha azma yao , idadi sawa na wanaowania kiti cha uwakilishi wa wanawake. Huku kipindi cha kampeni aidha kikitarajiwa kuanza rasmi tarehe io hiyo 29 mwezi huu wa Mei na kuendelea kwa siku sitini, mkuu huyo amewasihi wanasiasa kufanya kampeni za Amani na pia wanaowania viti mbalimbali kupewa fursa ya kuomba kura kwani wana haki kikatiba. Aidha ametoa wito kwa jamii kukumbatia na kuwapa nafasi wanawake na vijana am

MRADI WA SHARED FUTURES KUFAIDI VIJANA ELFU MOJA TANARIVER.

Image
Angalau vijana elfu moja na watu wazima kaunti ya Tanariver  wanatazamiwa kufaidi mradi wa miaka miwili na nusu wa majaribio unaolenga kuhusisha vijana katika Nyanja mbambali kwa malengo ya kukabili itikadi kali katika jamii. Mradi huo SHARED FUTURES ambao upo katika awamu ya pili utatekelezwa na mashirika tano yakiwemo Africa Youth Trust, Jamii action Centre,Samba sports Agenda, ADS pwani na CORDAID. Kulingana na Mohammed Mwachausa wa shirika la Samba sports Agenda  nia na madhumuni ya mradi huo utakaojumuisha mipango mbalimbali ya kuhusisha vijana kaunti hii ikiwemo maswala ya kilimo biashara, michezo na Sanaa pamoja na utangamano wa kidini ni kuhakikisha vijana wanahusishwa ili kuwaweka katika mazingira faafu yatakayowaondolea mafikira ya kujihusisha na makundi haramu na itikadi kali.  " Vijana wanapokuwa wanawachwa pekee yao na labda  wana ukiwa au upweke wanajihisi kuwa wamesukumwa na jamii  na serikali wajifanyie mambo kivyao mara nyingi wanakuwa na hasira na serikali, waza

MPUNGA HATARINI KUKAUKA BURA KWA KUKOSA MAJI

Image
Wakulima wa mpunga katika mashamba ya Bura  wamelalamikia kukauka kwa baadhi ya mashamba kutokana na ukosefu wa maji ya kutosha . Wakiongea na wanahabari mjini Bura , wakulima hao wanasema kuwa awali walipokuwa wakipanda mahindi hawakuwa na changamoto nyingi za maji ila tangia waanze kilimo cha mpunga kinachonoga kwa sasa wamekumbwa na upungufu wa maji mara kwa mara. "Tulipokuwa katika mradi wa kenya seed hatukushuhudia changamoto za maji lakini tangu tuanze mpunga tatizo la maji limekithiri kwasababu mpunga wahitaji maji mengi kunawiri." Alisema Lucy Wangari mmoja wa wakulima. Peter Muchai , mkulima mwingine amebaini kuwa baadhi ya wakulima katika mashamba hayo wanakadiria hasara kutokana na kukauka kwa mazao yao , tatizo kuu likiwa ukosefu wa maji ya kutosha mashambani. "Saa hii ukitembea kwa haya mashamba, mengi yameungua kwasababu ya ukosefu wa maji, tungepata maji ya kutosheleza kila mkulima hatungeomba msaada, shida haya maji tunapimiwa kama dawa." Amesema Mu