SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU KUCHINJA NG'OMBE 730 TANA RIVER AWAMU YA PILI YA MRADI WA SERIKALI
NA DENNIS MAITHYA Shirika la msalaba mwekundu kupitia serikali kuu limeanza awamu ya pili ya mpango wa kununua na kuchinja mifugo iliyodhoofika kaunti ya Tana River. Mratibu wa shirika hilo hapa Tana River Gerald Bombe amesema kuwa awamu hiyo ya pili ambayo ilianza tarehe mbili septemba inalenga kuchinja ng’ombe 730 kote kaunti hii. Katika awamu ya kwanza ya mpango huo iliyotamatika mwishoni mwa Julai, Bombe amebaini kuwa walichinja ng’ombe 525 kati ya 1,255 wanaolengwa kaunti nzima. “Katika awamu ya kwanza tulinunua na kuchinja ng’ombe 525. Delta ngo’mbe 84 na mbuzi 419, Tana Kaskazini ng’ombe 138 na mbuzi 131, Galole ng’ombe 138 na mbuzi 89.” Gerald Bombe- mratibu Redcross Tana River Kulingana na Bombe, Ng’ombe mmoja ananunuliwa kwa shilingi 15,000 na mbuzi au kondoo kwa shilingi 3,000. “Bei iliyowekwa kununua mifugo ni sawa katika kaunti zote zinazoshiriki mpango huu. Tunalenga wafugaji ambao wanahisi kuwa mifugo wao wamedhoofika kiasi kwamba hawaezi kustahimili hadi mv