TANA RIVER : BARAZA LA WANAHABARI NCHINI (MCK) LAHIMIZA USHIRIKIANO BAINA YA WANAHABARI NA UMMA
NA DENNIS MAITHYA . Mratibu wa baraza la kitaifa la wanahabari nchini (MCK) eneo la pwani Bi. Maureen Mudi ametoa wito kwa wanahabari kuzingatia kanuni za uanahabari msimu huu wa uchaguzi ili kuhakikisha usawa wa utoaji habari . Akizungumza katika kongamano lililokutanisha mck, wanahabari na washikadau wengine mjini Hola kaunti ya Tana River, Mudi ameelezea umuhimu wa ushirikiano baina ya asasi mbalimbali za jamii na wahabari , pamoja na umma kufahamu utendakazi wa wanahabari. "Kongamano hili linakutanisha wananchi wa mashinani na wanahabari kuwaeleza utendakazi wa wanahabari na majukumu ya vyombo vya habari ikiwemo utoaji wa habari kwa njia zinazostahili ." Mratibu huyo ameongeza kuwa baraza la kitaifa la wanahabari limeandaa misururu ya mafunzo kwa wanahabari uchaguzi mkuu unapowadia ili kuhakikisha wanaripoti matukio yanayohusiana na uchaguzi kwa njia ya usawa. "kama mck tumekuwa tukifanya mafunzo kwa wanahabari tunapoelekea uchaguzini.Himizo langu ni kwamba watoe