Posts

Showing posts from June, 2022

BURA: WATOTO WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA KWENYE MKONDO WA MAJI

Image
NA DENNIS MAITHYA Watoto wawili wa kike walio na umri wa miaka 13 na 14 mtawalia wameripotiwa kufariki dunia eneo la Bura gatuzi dogo la Tana North kaunti ya Tana River baada ya kuzama kwenye mkondo wa kupitishia maji maeneo ya Nanighi. Kulingana na ripoti ya idara ya polisi Bura tarehe 24 Juni, wawili hao wakazi wa kata ndogo ya BilBil walikuwa wanaogelea kwenye mkondo huo wa maji walipokutana na mauti. Ripoti hiyo imesema kuwa msichana wa kwanza wa miaka 13 alizama akiokoa mtandio uliokuwa unabebwa na wimbi la maji huku mwenzake wa miaka 14 akizama alipokuwa akijaribu kumuokoa . Miili yao ilichukuliwa kufuata taratibu za kisheria. Idara hiyo sasa imetoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanaandamana na mtu mzima wanapoenda kuchota maji au kuogelea katika mikondo hiyo ya maji iliyoko Bura  kwani kiwango cha maji hupanda na kushuka na kuweka hatari kwa watoto.

POLISI TANA RIVER WAOMBEWA UCHAGUZI MKUU UKIWADIA

Image
NA DENNIS MAITHYA Maafisa wa Polisi kaunti ya Tana River wamefanyiwa maombi maalum wanapojiandaa kuhudumia taifa katika uchaguzi mkuu wa Agosti tisa mwaka huu. Kamanda wa polisi gatuzi dogo la Tana Kaskazini Ali Ndiema amesema ibada hiyo ya maombi imewafaa sana maafisa wa polisi wanapojiandaa kwa uchaguzi mkuu nchini. Ndiema amesema kuwa nyakati za ibada angalau maafisa hunawiri ki imani na hata kisaikolojia kwani wanapotangamana na wenzao wanabadilishana hisia na mawazo. " Ibada hizi huwaleta maafisa wa polisi pamoja kupata baraka,kujengeka kiroho na hata kisaikolojia, hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzini tumejazwa nguvu na bila shaka tunarajia uchaguzi mwema."   Ali Ndiema(katikati) kamanda wa polisi gatuzi dogo la Tana North.  Aidha amebaini kuwa maafisa wamepewa mwongozo tosha wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao katika uchaguzi kama tume ya uchaguzi IEBC inavyoelekeza. "Tumezungumza na maafisa wetu na wanafahamu wanavyotakikana kufanya kazi kuhakikisha uchaguzi s

KAZI MTAANI YAREJEA.ZAIDI YA VIJANA 5,000 TANA RIVER KUFAIDI

Image
 Zaidi ya vijana elfu tano katika wadi 15 kaunti ya Tana River watanufaika na awamu ya tatu ya mpango wa Kazi mtaani. Akizindua mpango huo eneo la Mikinduni gatuzi dogo la Galole siku ya jumatatu tarehe 6 Juni , Kamishena wa kaunti Thomas Sankei amesema kuwa awamu hiyo itazingatia kuwafaidi watu wenye mahitaji maalum kuwakinga na changamoto za kiuchumi. kamishna wa Tana River Thomas Sankei akizindua kazi mtaani awamu ya tatu Sankei ameongeza kuwa mpango huo umejiri wakati mwafaka ambapo uchaguzi mkuu unawadia , akidokeza kuwa tofauti na awali vijana  pia watahusishwa katika mazungumzo ya kuleta amani na kutatua mizozo katika jamii. "Tunataka vijana wetu wawe mabalozi wema katika maswala ya maadili,kujenga amani na kutatua mizozo katika jamii.wakati huu wa uchaguzi tunataka tuelekeze watu hatutaki vurugu." wakiongozwa na Robert Buya vijana waliohudhuria wamepongeza serikali kwa kuregesha mpango huo kwani wangali wanatatizwa na changamoto za kiuchumi. Aidha amesihi serikali ku

MGOMBEA WA KITI CHA UWAKILISHI WA WANAWAKE ABUBUJIKWA NA MACHOZI KATIKA KITUO CHA IEBC

Image
NA DENNIS MAITHYA Mgombea wa kiti cha uwakilishi wa wanawake Tana River Bi. Mwanahamisi Omar alitekwa na hisia na kutokwa na chozi la furaha akikabidhiwa cheti na mkuu wa uchaguzi kaunti hiyo Yonah Ogalo. Mwanahamisi anayegombea kiti hicho kwa mara ya kwanza kwa tiketi ya chama cha Safina amesema kuwa pindi tu akikabidhiwa cheti hicho alimkumbuka marehemu baba yake ambaye alitamani sana kuwa naye kushuhudia ushindi wa mwanawe. Mwanahamisi Omar akipokezwa cheti na mkuu wa uchaguzi Yonah Ogalo "Nilipokuwa nakabidhiwa cheti nilitamani na kuhisi ningekuwa na baba yangu kando yangu.Hisia kidogo ya kumkumbuka ilinishika kwani ni siku kama ya tano hivi tangu nimpoteze."  Mwanahamisi ameahidi kuweka elimu ya mtoto wa kike kipaumbele akizingatia changamoto kama vile mimba na ndoa utotoni zinazowakumba watoto wa kike kaunti ya Tana River. "Sitakubali msichana kukatiza ndoto yake ya elimu kwasababu ya mimba .nitahakikisha wamesoma kwasababu wengi wametelekezwa na kuwachishwa shul